Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Viongozi wengine wa Serikali amefika msibani kwa malehemu Benard Membe kutoa salamu za pole kwa familia,ndugu jamaa na marafiki walio shiriki katika msiba huo.
DK.Samia amesema kufuatia msiba huo malehemu atakumbukwa kwa kazi alizozifanya kwa kipindi cha utumishi wake ikiwa ni pamoja na uwajibikaji bora na kusema malehemu alikuwa nguzo kuu kwa watanzania na mataifa mengine.
Dk.Samia amesema amekuwa na Membe katika nyakati tofauti katika baraza la Mawaziri na ndani ya kamati kuu ya Halmashauri ya chama cha mapinduzi kwa muda murefu.
Rais Samia amsema malehemu alikuwa muungwana mchapakazi aliyehamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi na wananchi wake.
Amesema kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa Taifa lake bali hata kwa mataifa mengine aliyowahi kuhudumu huku akisema mchango wa malehemu ni mkubwa kwa taifa la Tanzania hasa katika nyanja ya Diplomasia.
"Nimalizie kwa kukupa pole mjane wa malehemu na mdogo wangu Dolkas,Watoto wetu,ndugu jamaa na marafiki pamoja na wanalindi tuzidi kumuomba mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe amiina kwa waislam tuseme Innarillah wa Innarillah Rajillun
Tags
HABARI