Mwanamme mmoja anaekadiliwa kuwa na umli wa miaka 40 amepoteza maisha na wengine takribani watu 30 wakijeruhiwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam kufuatia mchezo uliokuwa ukichezwa leo 28 Mei 2023 kati ya Yanga dhidi ya USMA.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii amesema majeruhi wanaendelea vizuri wanamajeraha madogomadogo,wanaendelea kupatiwa vipimo huku akieleza kuwa Timu ya Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ilishilikiana kuangalia kama kutakuwa na majeruhi wengine.
Tags
HABARI