SHIRIKA LA UMEME TANESCO LAJENGA HISTORIA YA KWANZA TANZANIA


 SHIRIKA Umeme Tanzania (TANESCO) limeandika Historia ya kwanza kwa kusaini mkataba wa Mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya jua kwa kutumia Teknolojia ya Solar Photo Voltaic wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150 za umeme.

Hayo yamesemwa leo Mei 29,mwaka huu katika Ukumbi wa Morena Jijini Dodoma na Waziri wa Nishati January Makamba wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa kwanza nchini wa kuzalisha umeme wa jua megawati 50 utakao jengwa katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mhe.Makamba amesema mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza zitazalishwa megawati 50 na awamu ya pili zikitarajiwa kuzalishwa megawati 100 huku akibainisha kuwa mradi huo utatekelezwa na Kampuni ya SINOHYDRO CORPARATION kutoka nchina.

Pia ameseam hadi kukamilika kwa mradi huo ikiwemo ulipaji wa fidia kwa watakaopisha eneo la mradi itaghalimu jumla ya fedha kiasi cha shilling Bilioni 274.76.

Aidha amesema kusainiwa kwa mradi huo ni sehemu ya mipango ya mapinduzi katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo mseto katika sekta ya nishati nchini ili kufikia lengo la kuwa na megawati 5000 katika gridi ya Taifa ifikapo 2025.

Hali kadhalika awali Mhe.Makamba ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi juni mwaka huu ambapo utachukua takribani miezi 14 hadi kukamilika kwake.     

Previous Post Next Post