Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kumkamata mtuhumiwaa anaejulikana kwa jina la Isack Robertson mwenye umli wa miaka 45 na mkazi wa Sombatini Mkoani Arusha kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mke wake aitwae Jackline Mkonyi mwenye umli wa miaka 38 wa Sambotini Mkoani Arusha.
Hayo yamebainishwa leo
28 MEI,2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amesema
Mtuhumiwa huyo ameendelea kuhojiwa na pindi upelelezi utakapo kamilika jarada
litapelekwa Ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Jeshi la Polisi Mkoani
humo limetoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili
katika familia zao na sehemu nyingine kuacha mara moja huku likisema halitasita
kuwakamata na kuchukuliwa sheria watakaobainika na vitendo hivyo.
“Niwaombe wananchi
popote pale mlipo msifumbie macho vitendo viovu na pia musiache kutoa
ushirikiano pindi mnapoon tukio lolote ambalo si jema ili jeshi la Polisi
liweze kuwashughulikia waharifu na kukomesha vitendo hivi.
Tags
HABARI