Yanga watashuka dimbani leo kumenyana na USM Alger katika mchezo wa kwanza wa Fainali ya kombe la shirikisho (CAF) dulu hilo litapigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es saalam.
Akizungumza na Mapinduzi Digital kwenye uwanja wa shule ya Msingi Nkuhungu mmoja wa shabiki wa timu hiyo Efraim Lumumba amesema timu hio imekuwa na mwendelezo mzuri tangu msimu uanze ivyo imekamilika kila idara.
Amesema wachezaji wamepata mda wakutosha kupumzika baada ya kucheza mchezo wao wa nusu Fainali ya kombe la Azam Federation Cup Mkoani Singida kwenye uwanja wa CCM Liti nakuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa nusu Fainali ya kwanza.
Amesema USM Alger wajiandae kuondoka wakilia nahuzuni nzito watakapo ona wananchi wanapepelusha bendera ya
kijani huku wakitetema kwenye uwanja wa Mkapa kwa sababu maandalizi ya timu hiyo yanalizisha lengo nikupata alama wakiwa katika Dimba la Mkapa.
"Katika
mchezo huu tutahakikisha tunaonyesha uzalendo wetu wa kweli Usm Alger
tutawafunga na tutaendelea kutunza historia ya kuchukua kombe la hili laundi
hii tuna wapiga ndani nje kwetu tunabuluza natukienda kwao wembe ni
uleule''alisema Lumumba.
Amesema
yanga wasibweteke kwa sababu hawajui wapinzani wao wamejiandaa kwa nanmna gani
kuelekea kwenye Fainali hiyo na watatumia mbinu gani kwa sababu hawajawahi
kucheza nao mchezo wowote.
‘’USM Alger
ninavyo wajua katika michezo yao mingi huwa wanatumia mbinu ya kujilinda sana
ili wapinzani wao wasiweze kutikiswa nyavu zao kwahiyo wanajangwani kazi ipo na
siyo kidogo''alisema masawe