Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amesema serikali imeanza kutekeleza mpango wa kukifanya chuo cha utumishi wa umma kampasi ya Tabora kiweze kutumika kuwanoa makatibu mahususi na watunza kumbukumbu kwenye ngazi ya shahada.
Rais Samia amesema hayo leo wakati wa kufunga mafunzo ya pamoja ya chama cha watunza kumbukumbu na nyaraka [TRAMPA] na chama cha makatibu mahususi Tanzania [TAPSEA]katika viwanja vya fumba Zanzibar.
Aidha Rais Samia amesema lengo la kupandisha hadhi chuo hicho ni kuandaa watendaji wenye uweledi na viwango vya juu kwa kutumia mitaala mipya.
Rais Samia pia amewasisitiza watunza kumbukumbu na nyaraka na makatibu mahususi kufanya kazi kwa nidhamu,uadilifu na kuzingatia misingi ya utunzaji siri, miongozo na kuheshimu mipaka ya kiutendaji.
Vile vile Rais Samia amewahimiza kufanya kazi kwa uweredi katika taaluma zao na kushirikiana katika utekerazaji wa majukumu yao.
Katika hatua nyingine Rais Samia amewaelekeza mawaziri wenye dhamana ya utumishi wa umma na utawala bora kuzungumuza na waajili katika sekta binafsi ili kuwaruhusu na kuwasaidia wanataaluma kushiriki mafunzo hayo.
Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kuwaleta pamoja makatibu mahususi na watunza kumbukumbu na nyaraka kwaajili ya kupata mafunzo maalumu yenye kuwaongezea tija na ufanisi.