Rais Samia ameyasema hay oleo nchini Zanzibar
aliposhiriki katika kuhitimisha mkutano wa kitaaluma wa chama cha makatibu
mahususi na Menejimenti ya kutunza kumbu kumbu ya APRA na TAPSEA ambapo
amewapongeza viongozi hao kwa kuendelea kusimamia sekta hiyo.
Dk.Samia pia amewasihii viongozi hao kuendelea
kutatua changamoto zinapojitokeza huku akiwataka watumishi wa kada ya Elimu
kuchangamkia fursa kwani inawajenga kitaaluma na kuwapa nafasi ya kupumzika.
Dk.Samia amewataka wafanyakazi kwenda sawa na viapo walivyo apa ili kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kumtakaa Waziri wa utumishi na Waziri anaeshughulika na ajiri kuzungumza na waajiri kuyatekeleza vyema majukumu yao.
“Kama mwanadamu unataka kupumzika Mawaziri
lishughulikieni hilo,nimesikiliza kiapo chenu hapa na mzlivyosema lakini hii
ndio fursa pekee kwa kada hizi kutoka nje ya Ofisi zao wakitoka ni wakati wa
likizo lakini likizo waenda Vijijini kwa wazazi kwa hiyo ile wapiti kupmzika
wanapata matatizo tele yanawasubiri labda wananchopata ni kubadilisha mazingira
tuu.
Katika hatua nyingine Dk.Samia amewakumbusha na
kuwataka kusimamia suala la kuongezwa kwa hadhi ya Chuo cha Utumishi Kampasi ya
Tabora ambapo amesema awali yalitolewa maagizo ya kuongezwa hadhi ili kiweze
kuandaa watendaji wenye uweledi na viwango vya juu.
Pia Rais Samia amempongeza Waziri kwa kukamilisha
agizo hilo huku akimtaka kukamilisha suala la mitaala kwa wakati ili Chuo
kianze kazi kama ilivyopangwa.
Amesema kuhusu Chuo cha Maarifa kilichopo Jijini
Dodoma kitawekwa jina la Samia hadi pale ujenzi utakapo kamilika”Sisi waswahili
hatutoi jina mpaka motto azaliwe si waswahili wa zamani,sasa subirini kituo
hiki kikamilike tukione kilivyo tutaamua jina gani,”Dk.Samia
Aidha Dk.Samia amesema mfumo uliopo utaendelea
kujenga taasisi imara.