Rais wa Jamuhurin ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa,uteuzi Mkuu wa Mkoa,Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na Uteuzi wa Mkuu wa Wilaya.
Rais Samia amefanya uteuzi huo leo Mei 23 mwaka huu ambapo amemteua Mhe.Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.Mhe.Mtanda ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora ambapo anachukua nafasi ya Meja Jeneral Suleiman Mungiya Mzee.Meja Jeneral Mzee amepangiwa majukumu mengine.
Mhe.Queen Cathibert Sendiga amehamishwa kuwa Mkuu wa Mokoa wa Manyara.Mhe.Sendiga alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa anachukua nafasi ya Mhe.Makongoro Nyerere ambae amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Pia amemteua Bw.Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulambo.Kihongosi anachukua nafasi ya Mhe.Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Uapisho wa Mkuu wa Mkoa Mpya utafanyika tarehe 24 Mei 2023 saa kumi kamili jioni katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.