HATIMA YA LIG DARAJA LA KWANZA CHAMPIONISHIP 2022/23 MEI 13,2023


 Lig Daraja la kwanza Championship 2022/23 imeailishwa leo kufuatia mchezo wa KitayosCe dhidi ya Afrikan Sports kwa mchezo huo KitayosCe imefanikiwa kupanda daraja lig kuu ya NBC 2023/2024.

Kitayosce imefikisha alama 60 tofauti ya alama moja na Pamba Fc ambayo imemaliza nafasi ya tatu huku ikiwa na alama 59 wakati JKT Tanzania ambao ndio mabingwa wa ligi hiyo wakiwa na alama 63.

Kitayosce wanaungana na JKT Tanzania kupanda lig Kuu ya NBC moja kwa moja bila ya kucheza Palay off.

Pamba Fc imemaliza nafasi ya tatu na Mashujaa Fc nafasi ya nne,kwa mjibu wa kanuni za Lig hiyo Timu hizo zitacheza Play off kwa nia ya kupanda Lig Kuu kwa mwaka 2023/24.


Previous Post Next Post