TEA YAMSHANGAZA MZAZI BAADA YA MWANAE KUONYESHA UMAHIRI MKUBWA WA USHONAJI



Na Mwandishi Wetu, Da es Salaam.


Bi. Catalina Joseph, mzazi, amemtembelea mwanae mwenye ujuzi wa kushona katika banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kushangazwa na kiwango kikubwa cha ubunifu na umahiri alioonyesha katika kazi zake.


Akizungumza baada ya kujionea bidhaa mbalimbali zilizoshonwa na mwanae, Bi. Catalina amesema hakuwa akitarajia mafunzo ya amali yangeleta mabadiliko ya haraka na makubwa kiasi hicho katika maisha na ujuzi wa mtoto wake.


Ameipongeza pia TEA kwa kuweka mazingira wezeshi yanayowasaidia vijana kujifunza kwa vitendo na hatimaye kujitegemea kiuchumi kupitia sanaa ya ushonaji.


Banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni wengi wanaotembelea maonesho hayo.




🚨Full Video Inapatikana Katika YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA
Previous Post Next Post