KIKAO KAZI CHA KUHUISHA NYENZO ZA MAFUNZO YA MENEJIMENTI YA MATUKIO YA DHARURA YANAYOATHIRI AFYA YA JAMII.


Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Shirika la CIHEB pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, inaendesha kikao kazi cha kuhuisha nyenzo za mafunzo ya Menejimenti ya Matukio ya Dharura Yanayoathiri Afya ya Jamii (Public Health Emergency Management Training) kuanzia tarehe 8 ,Juni,2026.


Kikao kazi hicho kinalenga kuboresha nyenzo za mafunzo kulingana na  mahitaji ya sasa ya nchi katika kujiandaa, kugundua mapema, kukabiliana kwa haraka na kudhibiti magonjwa ya mlipuko pamoja na dharura nyingine zinazoweza kuhatarisha Afya ya jamii.


Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuendelea kuimarisha mfumo wa ulinzi wa afya ya umma kwa kujenga uwezo wa watumishi wa sekta ya afya na sekta nyingine zinazohusika na usimamizi wa dharura katika ngazi zote za utekelezaji.


Uhuishaji wa nyenzo hizi unazingatia uzoefu uliopatikana katika kukabiliana na matukio mbalimbali  yaliyowahi kutokea nchini, na miongozo ya  menejimenti ya dharura za afya.


Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo imara wa utayari na mwitikio wa haraka kwa matukio ya dharura yanayoathiri afya ya jamii, hatua itakayochangia kulinda afya, ustawi na maisha ya wananchi.











🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.
Previous Post Next Post