KIKAO KAZI CHA KUANDAA NYENZO SANIFU ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA MTAALA WA NYONGEZA WA UFUATILIAJI WA MAGONJWA YALIYOPEWA KIPAUMBELE CHAANZA MOROGORO.


Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga, Sehemu ya Epidemiolojia, kwa ufadhili wa Mfuko wa Pandemic Fund, imeanza kikao kazi cha kuandaa nyenzo sanifu za kufundishia na kujifunzia Mtaala wa Nyongeza wa Ufuatiliaji wa Magonjwa Yaliyopewa Kipaumbele nchini.


Kikao hicho kilichoanza leo tarehe 8 Juni, 2026 mkoani Morogoro, kinawakutanisha wataalamu kutoka Idara ya Mafunzo ya Wizara ya Afya pamoja na wataalamu kutoka vyuo vya afya vya kada za kati ili kuandaa nyenzo zitakazojumuishwa katika mitaala ya vyuo vya afya na kutumika kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii na kada za kati katika ufuatiliaji, ugunduzi na utoaji wa taarifa za magonjwa yaliyopewa kipaumbele.


Hatua hii ni sehemu ya jitihada za kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa na kuongeza utayari wa nchi katika kukabiliana na milipuko na dharura za afya ya umma.












🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.
Previous Post Next Post