MZEE WA MIAKA 79 HAOFIA KUULIWA NA MWANAE KISA KURITHI MASHAMBA

 

Mzee Peter Samwel aliyevaa koti akiteta jambo na mwanae mkubwa wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya kutishiwa kuuliwa na mwanae wa sita Andason Peter anayelazimisha kukabidiwa mashamba kama sehemu ya urithi.

Na Mwandishi Wetu, MANYONI📍


MZEE Peter Samwel (79) ameeleza masikitiko yake ya kutishiwa kuuliwa na mwanae Andason Peter kwa madai ya kulazimishwa kumpatia mwanae shamba la  kulima.


Kutokana na hali hiyo  ameiomba viongozi wa  Serikali ya Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni Mkoani  kumsaidia kulinda maisha yake kutokana na baada ya  mtoto wake Andason kulazimisha kupewa mashamba ya urithi.


Mzee Peter amesema kuwa pamoja na kuwa mzee lakini amekuwa akitishiwa kuuliwa na mwanaye Andason kwa kumlazimisha kupewa ardhi kwa lazima.


Mzee Peter amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano mtoto wake huyo amekuwa akimlazimisha kumlazimisha kumpa eneo lake kama sehemu ya uridhi jambo ambalo limeendelea kuzua mgogoro wa kifamilia unaotokana na suala la umiliki wa ardhi.


Mzee huyo mwenye watoto wa 9 huku mtuhumiwa akiwa mtoto wa sita mesema kuwa Andasani amekuwa mwiba katika familia kwani amechukua hatua hata ya kuvuruga mazao ambayo mzee huyo alikuwa ameisha yapanda.


Hata hivyo mzee huyo ameeleza kuwa kutokana na vitisho vya mwanae vya kutaka kumuua kumemsababishia kupata ugonjwa wa mshtuko wa damu.


Katika hatua nyingine mzee huyo ameeleza kumlipoti katika kituo cha polisi kata ya Kintinku ambapo amesema kuwa huko ndiko anakotarajia kupata uponyaji wake.


Mzee peter kutokana na kutishiwa na mwanaye kwa ajili ya kutaka kuporwa ardhi yake amesema ili kuweka ulinzi wa kisheria atalazimika kufungua kesi ya ardhi katika baraza la ardhi la kata ya kintinku.


Hata hivyo viongozi wa kata pamoja na kijiji wamekiri kulifahamu jambo hilo ambalo limedumu kwa miaka mitano sasa.


🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA

Previous Post Next Post