Na Carlos Claudio, Dodoma.📍
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amewataka watumishi wa umma katika wizara hiyo kuacha mara moja vitendo vya maovu dhidi ya wananchi wanaohudumiwa katika ofisi za ardhi na badala yake kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo.
Akizungumza leo January 23,2026 jijini Dodoma katika kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi nchini, Dkt. Akwilapo amesisitiza matumizi sahihi ya sheria na kanuni za ardhi kama njia ya kutokomeza migogoro ya ardhi inayoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, amewataka watumishi kutoa ufafanuzi wa wazi kuhusu malalamiko yanayotolewa na wananchi pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu ya masuala ya ardhi kwa jamii ili kuongeza uelewa na kupunguza migogoro isiyo ya lazima.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ardhi (Mb), Kaspar Mmuya, amewahimiza watumishi wa umma kutunza siri za serikali na kuhakikisha wanaacha alama nzuri wanapostaafu au wanapobadilishiwa majukumu, akisisitiza umuhimu wa maadili na uwajibikaji katika utumishi wa umma.
🚨Full Video Inapatikana Katika YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.











