Na Carlos Claudio, Dodoma.📍
Serikali imetakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha kina mama, hususan wale waliopo majumbani wenye juhudi za kufanya biashara lakini wanakwamishwa na ukosefu wa mitaji pamoja na masharti magumu ya mikopo kutoka taasisi za kifedha.
Wito huo umetolewa leo Januari 25, 2026 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Jenipher Mall, Jenipher Samuel, wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya la biashara linalojihusisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali za majumbani ikiwemo vyombo vya ndani, mapambo ya ndani na mahitaji mengine ya kifamilia.
Jenipher amesema kuwa wanawake wengi wana ndoto na nguvu ya kufanya biashara, lakini hukwama wanapohitaji mtaji kwa sababu benki na taasisi nyingi za fedha zinahitaji dhamana zisizohamishika kama nyumba au viwanja ambavyo wengi hawana.
“Serikali itusaidie kupata mifumo rafiki ya mikopo pasipo masharti magumu ili kuepusha kuzikwa kwa ndoto za wajasiriamali wenye uwezo na juhudi,” amesema Jenipher.
WANAWAKE WAKIFANIKIWA HAWAPUUZI FAMILIA
“Zipo familia nyingi ambazo wanawake wamefanikiwa lakini bado ni wake bora na mama wazuri. Mafanikio ya mwanamke hayamaanishi kuvunjika kwa familia,” amesema.
Ametoa wito kwa wanaume kuwa na imani kubwa kwa wanawake zao wanapoonesha juhudi za kupiga hatua kimaisha, akisema kuwa hilo ni nguzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
MUME WANGU NI NGUZO YA MAFANIKIO YANGU
“Kama nisingepata imani yake na ruhusa ya kutoka nje kuonesha uwezo wangu, nadhani kile mnachokiona leo kisingekuwepo,” amesema.
SAFARI YA JENIPHER MALL KUTOKA MILIONI TATU HADI KUWA MALL
Kwa msaada na ushauri alioupata, alianza kuuza bidhaa zake hatua kwa hatua kuanzia maeneo ya vichochoroni hadi kufikia hatua ya nne ya ukuaji wa biashara ambayo sasa ni Jenipher Mall.
BIDHAA BORA KWA BEI RAFIKI KWA KILA MTANZANIA
“Jenipher Mall ina kila aina ya bidhaa za majumbani, zenye ubora wa juu lakini kwa bei ya chini na rafiki kwa kila mmoja,” amesema.
Ameongeza kuwa mall hiyo imeleta bidhaa ambazo awali hazikupatikana jijini Dodoma, hali iliyowalazimu wananchi wengi kuagiza kutoka Dar es Salaam.
MKAKATI WA KUFIKIA TANZANIA YOTE NA MNADA WA BEI FUPI
Amesema mnada huo utawarahisishia wateja waliopo mikoani ambao hawana imani ya kuagiza bidhaa kwa njia ya mtandaoni.
UJUMBE KWA WAJASIRIAMALI WADOGO
“Ukijitoa, ukawa mwaminifu na mwenye nidhamu ya fedha, mafanikio yanawezekana,” amesema.
![]() |
![]() |
🚨Full Video Inapatikana Katika YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA


















