Na Carlos Claudio, Dodoma.📍
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Mustapha Rajab, ametoa wito kwa Waislamu na wananchi kwa ujumla kuepuka matumizi yasiyo sahihi ya neno haki yanayoenezwa kupitia mitandao ya kijamii, akisema kuwa tafsiri potofu za dhana hiyo zimekuwa chanzo cha kuchochea migawanyiko na vurugu zisizo na msingi.
Akizungumza leo, Desemba 12, 2025, katika hutuba ya swala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Gaddafi jijini Dodoma, Sheikh Dkt. Mustapha alisema baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha maana ya haki na kuitumia vibaya kwenye majukwaa ya mtandaoni, hatua inayoweza kuathiri amani ya jamii.
“Sheikh alisema imefika wakati kila Muislamu na Mtanzania kwa ujumla kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu, kwa sababu tafsiri zisizo sahihi za haki zimekuwa zikichochea migawanyiko ambayo haina msingi katika misingi ya dini wala maadili ya taifa.”
Aidha, aliwasisitiza vijana wa Kiislamu kujikita katika kumcha Mungu na kuepuka kushiriki maandamano yasiyo na tija, akisema vitendo hivyo vinaweza kuhatarisha tunu ya amani ambayo taifa limeijenga kwa muda mrefu.
“Sheikh Dkt. Mustapha alibainisha kuwa amani ni rasilimali muhimu inayopaswa kulindwa na kila mmoja. Aliongeza kuwa maandamano yasiyo na sababu za msingi yamekuwa yakitumiwa na baadhi ya watu kuibua vurugu na kuathiri maisha ya wananchi wasiohusika.”
Wito wake unakuja katika kipindi ambacho matumizi ya mitandao ya kijamii yameongezeka, huku baadhi ya watumiaji wakisambaza taarifa zenye kuchochea hisia kali na kuathiri mshikamano wa kitaifa.
Sheikh Dkt. Mustapha aliwataka Waislamu na Watanzania wote kuendeleza utamaduni wa kujadiliana kwa hoja, kuheshimiana na kulinda amani ambayo imeendelea kuwa nguzo ya maendeleo ya taifa.
🚨Full Video Inapatikana Katika YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.



