SHEIKH WA DODOMA: ACHENI SIASA, HUDUMIENI WAUMINI KIROHO



Na Mwandishi wetu, Dodoma.📍


Viongozi wa Dini wameshauriwa Kusimama kwenye Nafasi zao kwa kufuata Msingi ya dini na Kuachana na masuala ya siasa ili kuepuka uchochezi na badala yake kuwahudumia kiroho waumini na kuhubiri Amani. 


Ushauri huo umetolewa na SHEIKH wa Mkoa wa Dodoma, Alhaji Mustafa Rajab wakati wa Ibada ya  Ijumaa katika Msikiti wa GADDAFI ambapo amesisitiza viongozi wa Dini kubaki kwenye mipaka yao ya Kazi ya kiimani na Kuacha kujihusisha na masuala ya Siasa kuepuka kuwapa waumini wao mkanganyiko.


Sheikh rajab, amewaasa watanzania kuwa wasikivu na watii kwa kuheshimu mamalaka na maagizo yanayotolewa na Viongozi wa Serikali ili kuendelea kudumisha Amani na Utulivu katika Taifa.




Kwa upande wao Asia abdallah na Karimu Rajabu waumini waliohudhuria ibada hiyo wamesema wamepata Darasa lenye ujumbe mkubwa ambao utawastawisha katika kudumisha amani miongoni mwa wanajamii na kuondosha dhana mbaya zilizobeba uchochezi wenye viashiria vya uvunjifu wa Amani.


🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post