Na Carlos Claudio, Dodoma.📍
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limefanya maboresho mapya ya miongozo yake ya elimu ili kuhakikisha vijana wanaomaliza masomo katika vyuo vya ufundi nchini hawakumbwi na changamoto ya ukosefu wa ajira.
Ndunguru alibainisha kuwa mabadiliko hayo ni sehemu ya jitihada endelevu za serikali kuhakikisha elimu ya ufundi inaendana na mahitaji ya viwanda, sekta binafsi pamoja na mabadiliko ya teknolojia duniani.
“Athari ya moja kwa moja ya maboresho haya ni kukuza soko la ajira kwa wanafunzi, kuwaongezea uwezo wa ushindani, na kuhakikisha kwamba wahitimu wanakuwa tayari kuingia kwenye dunia ya kazi bila changamoto,” alisema Dkt. Lingwanda.
Aidha, baraza hilo limeahidi kuendelea kusimamia ubora wa elimu katika vyuo vya ufundi nchini pamoja na kupanua wigo wa udahili ili kutoa fursa zaidi kwa vijana kupata elimu na ujuzi utakaowawezesha kujitegemea.
Warsha hiyo imetoa taswira mpya ya mwelekeo wa elimu ya ufundi nchini, ikionyesha dhamira ya dhati ya NACTVET katika kuleta mageuzi chanya yatakayochochea maendeleo endelevu ya kiuchumi kupitia nguvu kazi iliyobobea katika ujuzi.






