𝐁𝐚𝐫𝐚𝐳𝐚 𝐥𝐚 𝐌𝐚𝐰𝐚𝐳𝐢𝐫𝐢 𝐥𝐢𝐥𝐢𝐥𝐨𝐭𝐚𝐧𝐠𝐚𝐳𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐌𝐡. 𝐑𝐚𝐢𝐬 𝐒𝐚𝐦𝐢𝐚 𝐒𝐮𝐥𝐮𝐡𝐮 𝐇𝐚𝐬𝐬𝐚𝐧



Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza baraza jipya la mawaziri, likihusisha wizara 27, huku akitimiza ahadi yake ya kuunda wizara kamili ya vijana.


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa nchi, wizara hiyo itakuwa chini ya ofisi yake na itaitwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana na kwamba Joel Nanauka ameteuliwa kuiongoza.


Rais Samia ametangaza baraza hilo leo, Jumatatu Novemba 17, 2025 katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.


Sambamba na wizara hiyo, pia amefanya marekebisho madogo na kuunda Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano.


“Atakayeshika nafasi hiyo atakuwa na kazi ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali kuhakikisha mahusiano mazuri,” amesema.


Aidha, marekebisho mengine yameshuhudiwa katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na sasa imehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu. 


Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

👔 Waziri - Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete

👩‍💼 Naibu - Regina Ndege Kwarai

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji


👔 Waziri - Prof. Kitila Mkumbo

👩‍💼 Naibu - Pius Steven Chaya


Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana

👔 Waziri - Joel Nanauka


Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

👔 Waziri - Mh. Mhandisi Hamadi Masauni

👩‍💼 Naibu - Dkt. Festo Dugange


Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu

👔 Waziri - Mh. William Lukuvu

👩‍💼 Naibu - Ummy Nderiananga


Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano

👔 Waziri - Mh. Deus Sangu

👩‍💼 Naibu - Mh. Rahma Riadh Kisuo


Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

👔 Waziri - Mh. Prof. Riziki Sailas Shemdoe

👩‍💼 Naibu - Mh. Reuben Nhamanilo (Elimu)

👩‍💼 Naibu - Mh. Dr. Jaffar Rajab Seif (Afya)


Wizara ya Fedha

👔 Waziri - Mh. Balozi Khamis Musa Omar

👩‍💼 Naibu - Mh. Laurent Deogratius Luswetula

👩‍💼 Naibu - Mh. Mshamu Ally Munde


Wizara ya Mambo ya Nje

👔 Waziri - Mahmood Thabit Kombo

👩‍💼 Naibu - Dkt. Ngwaru Jumanne Magembe

👩‍💼 Naibu - Mh. James Kinyasi Millya


Wizara ya Mambo ya Ndani

👔 Waziri - Boniface Simbachawene

👩‍💼 Naibu - Denis Lazaro Londo


Wizara ya Kilimo

👔 Waziri - Daniel Chongolo

👩‍💼 Naibu Waziri - Mh. David Silinde


Wizara ya Maji

👔 Waziri - Mh Juma Aweso

👩‍💼 Naibu Waziri - Mh. Kundo Andrew Mathew


Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

👔 Waziri - Mh. Raymond Simon Nyansao


Wizara ya Ujenzi

👔 Waziri - Abdallah Ulega

👩‍💼 Naibu - Mh. Godfrey Msonge


Wizara ya Uchukuzi

👔 Waziri - Prof Makame Mbarawa

👩‍💼 Naibu - Mh. David Mwakiposa


Wizara ya Viwanda na Biashara

👔 Waziri - Mh. Judith Salvio Kapinga

👩‍💼 Naibu - Mh. Patrobas Katambi


Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

👔 Waziri - Mh. Angela Kairuki

👩‍💼 Naibu - Mh. Sweetbert Zakaria Mkama


Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

👔 Waziri - Dorothy Gwajima

👩‍💼 Naibu - Mh. Marry Mahundi


Wizara ya Afya

👔 Waziri - Mohammed Mchengerwa

👩‍💼 Naibu - Dkt. Florance George Samizi


Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia

👔 Waziri - Prof. Adolf Mkenda

👩‍💼 Naibu - Wanu Hafidh Ameir


Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

👔 Waziri - Dkt. Leonard Akwilapo

👩‍💼 Naibu - Kasper Kasper Muya


Wizara ya Mali Asili na Utalii

👔 Waziri - Mh. Asha Kijaji

👩‍💼 Naibu - Hamad Hassan Chade


Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

👔 Waziri - Prof. Palamagamba Kabudi

👩‍💼 Naibu - Hamisi Mwinjuma

👩‍💼 Naibu - Paul Makonda


Wizara ya Mifugo na Uvuvi

👔 Waziri - Dkt. Bashiru Ally Kakurwa

👩‍💼 Naibu - Mh. Ngwasi Damas Kamani


Wizara ya Madini

👔 Waziri - Anthony Peter Mavunde

👩‍💼 Naibu - Mh. Dkt. Steven Lemomo Kiruswa


Wizara ya Nishati

👔 Waziri - Mh. Deogratius Ndejembi

👩‍💼 Naibu - Salome Makamba


Wizara ya Katiba na Sheria

👔 Waziri - Mh. Juma Homera

👩‍💼 Naibu - Zainab Athuman Katimba

Previous Post Next Post