Na Carlos Claudio, Dodoma.📍
Wakazi wa Jiji la Dodoma wamehimizwa kujenga utamaduni wa kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kununua kompyuta, ili kuepuka kufanya maamuzi yasiyo sahihi yanayoweza kuathiri utendaji wa kifaa na matumizi yao ya kila siku.
Ushauri huo umetolewa jijini Dodoma na Mtaalamu wa Kompyuta kutoka Pick Point Computers, Bw. Justine Majanja, wakati akizungumza na Washindi Media ambapo amewafundisha watumiaji wa kompyuta na wateja namna bora ya kuchagua kifaa kulingana na matumizi yao.
Bw. Justine ameeleza kuwa jambo muhimu zaidi la kuzingatia kabla ya kununua kompyuta ni aina ya matumizi ya mtumiaji, kwa kuwa kila kompyuta hutengenezwa kulingana na mahitaji maalumu.
“Kabla hujanunua kompyuta, jiulize ni kwa matumizi gani? Kazi za ofisini, ubunifu, michezo, au masomo? Hilo ndilo jambo la msingi kabla hujaangalia mambo mengine ya kiufundi,” amesema Justine.
![]() |
Aidha, alitaja mambo mengine muhimu yanayopaswa kuzingatiwa kuwa ni uwezo wa kompyuta kufanya kazi kwa wakati mmoja (RAM), uhifadhi wa taarifa (Storage – SSD au Hard Disk), na mengineyo kama processor, operating system, ubora wa betri, na miunganisho (connectivity) ikiwemo Type-C, USB 3.0, na HDMI.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, mwaka 2025 unahitaji watumiaji kuwekeza katika kompyuta zenye teknolojia ya kisasa hasa zinazotumia SSD, ambazo hutoa matokeo mazuri na kasi katika utendaji.
“Tunashauri pia wateja kutumia betri kwa umakini. Ukishachaji kompyuta hadi 100%, ni vizuri kuiondoa kwenye chaji ili kuongeza muda wa maisha ya betri. Na ni muhimu kutumia original adaptor pekee,” aliongeza.
Mbali na hilo, alisisitiza umuhimu wa kuwa na Windows halisi (genuine) pamoja na antivirus kwa ajili ya usalama wa kifaa na taarifa binafsi za mtumiaji.
Kwa upande mwingine, Pick Point Computers imejipambanua kuwa kituo cha huduma bora na za uhakika za kompyuta jijini Dodoma, ikitoa ushauri wa kitaalamu kabla ya mteja kununua kifaa.
“Tunakukaribisha Pick Point Computers. Toa maelezo ya matumizi yako, tutakushauri vizuri na kukupatia kompyuta sahihi kwa kazi zako za sasa na miaka ijayo, tukizingatia mabadiliko ya teknolojia,” alisema Justine.
Pick Point Computers pia inatoa huduma za software installation, ushauri wa matumizi, na mauzo ya laptops, desktops, vishkwambi, mabegi, na vifaa vyote vya kompyuta kwa bei nafuu kuanzia shilingi laki mbili.
Huduma nyingine ni pamoja na warranty kuanzia miezi 6, msaada wa wateja saa 24, na malipo kwa njia mbalimbalikama cash, simu, benki, au mpango wa kulipa kidogo kidogo kulingana na uwezo wa mteja.
Duka hilo linapatikana barabara ya 11, mkabala na Decca Poly Clinic, jijini Dodoma. Wateja wanaweza kuwasiliana kupitia namba 0788 186 858 au kwenye mitandao yote ya kijamii kwa jina pickpoint_computers pamoja na WhatsApp Channel yao rasmi.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.
















