Na Mwandishi Wetu, Dodoma.📍
Bwana Zuberi Omari Mwijuma, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya Majengo, jimbo la Dodoma Mjini, amefunga ndoa na Bi Hamida Harith Said katika hafla ya kihistoria iliyofanyika Oktoba 10, 2025.
Ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Badawiya, uliopo eneo la Mailimbili kituo cha CCM, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka kata ya Majengo.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Iddy Rajabu Maumba, Katibu wa Kata, Onyango David Charles Lusinde Amvaye, ambaye ni Muenzi wa Kata, pamoja na Mlewa Christopher Mahewa, Katibu wa UWT wa kata hiyo.
Akizungumza baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, Bwana harusi Zuberi Mwijuma alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa kata ya Majengo na Dodoma kwa ujumla kujotokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025, kushiriki katika uchaguzi mkuu.
“Ni muhimu sana tujitokeze kwa wingi siku hiyo ili tuchague viongozi wa maendeleo, ikiwemo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya urais, Mhe. Pascal Chinyele kwa ubunge wa Dodoma Mjini, pamoja na madiwani wa chama cha mapinduzi,” alisema Mwijuma kwa furaha.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa maharusi hao, ambapo furaha, nyimbo za harusi na salamu za pongezi zilitawala siku nzima.
Wakazi wa kata ya Majengo wamepongeza ndoa hiyo na kumtakia Bwana harusi Mwijuma maisha mema ya ndoa pamoja na mafanikio katika jitihada zake za kuleta maendeleo katika jamii.









