KATOTO TENNIS ACADEMY YAANDAA MASHINDANO YA KUSAKA VIPAJI DODOMA


 

Na Carlos Claudio,

Dodoma, Septemba 6 — Katoto Tennis Academy imeandaa mashindano ya siku mbili jijini Dodoma kwa lengo la kusaka na kukuza vipaji vya mchezo wa tennis kwa watoto.


Mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya Tennis vya Njedengwa yameshirikisha watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 12 kutoka mikoa minne ya Arusha, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa waandaaji, lengo kuu ni kuwapa nafasi watoto chipukizi kuonyesha uwezo wao, kukuza ushindani wa kimichezo na kuandaa kizazi kipya cha wanatenisi wa Tanzania.








🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post