JWT PWANI IMEPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KWA KUPUNGUZA UTITIRI WA KODI


Na Mwandishi, Wetu Pwani.


Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Pwani imepongeza serikali kwa kupunguza changamoto kwenye masuala ya ulipaji kodi na tozo mbalimbali.


Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Athuman Said alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari juu ya mazingira ya ufanyaji biashara amesema kuwa utendaji kazi wa taasisi zinazohusika na utozaji kodi mbalimbali za serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato (TRA) imeweka mazingira rafiki tofauti na miaka ya nyuma.


Said amesema kuwa serikali kupitia TRA kwa sasa wanashirikiana vizuri na wafanyabiashara katika ulipaji kodi kwa utaratibu mzuri bila ya bughudha tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo ilifikia hatua wafanyabiashara walikuwa wakifunga maduka na kukimbia.


Amesema kuwa zamani ilifikia hatua walikuwa wakifungiwa maduka kwa kushindwa kulipa kodi lakini kwa sasa hata kama mfanyabiashara kashindwa kulipa kodi wanakaa mezani na anapewa muda wa kueleza atalipa kwa njia gani au kwa muda fulani atakapokuwa amepata fedha.


"Ukusanyaji kodi kwa sasa umekuwa ni rafiki siyo wa kubughudi wafanyabiashara bali ni kwa kushirikiana hali ambayo inawafanya wafanyabiashara kulipa kodi bila ya usumbufu,"amesema Said.



Naye mwenyekiti wa Soko la Loliondo Mohamed Mnembwe amesema kuwa wanamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.


Mnembwe amesema kuwa kauli aliyoitoa Rais ya kutaka wafanyabiashara wasibughudhiwe imewafanya wafanyebiashara zao bila ya changamoto hivyo kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi.



Kwa upande wake Steven Shehiza amesema kuwa ameomba serikali itanue wigo kwa wafanyabiashara wa ndani waweze kufanyabiashara nje ya nchi ili kuongeza pato la Taifa.






🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post