MAKALLA: WAGOMBEA CCM WATULIE MPAKA JULAI 28


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amewataka wagombea wote wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kutulia na kusubiri kwa subira hadi mchakato wa uteuzi utakapokamilika.


Akizungumza leo Jumamosi Julai 19, 2025, katika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, Makalla amesema kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kitafanyika Julai 26, kikitanguliwa na kikao cha Kamati Kuu.


“Uteuzi wa mwisho utafanyika Julai 28. Wagombea wawe watulivu, kazi ya kuchambua ni kubwa kutokana na idadi yao, na tunataka kuhakikisha tunatenda haki,” amesema Makalla.


Amesisitiza kuwa baada ya uteuzi huo, wagombea waliofanikiwa wataelekea kwenye hatua ya kura za maoni.



🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post