DKT. SAMIA AZINDUA RASMI DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 17, 2025, amezindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050,akibainisha kuwa  imebeba matarajio ya Watanzania kwa miongo ijayo na hivyo utekelezaji wake lazima uwe wenye tija, unaopimika na unaozingatia uhalisia wa maisha ya watu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliyofanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, vyama vya siasa, mabalozi na wadau wa maendeleo,ambapo amesema inalenga kuipeleka  Tanzania kwenye uchumi wa kati wa juu, kwa msingi wa maendeleo jumuishi, usawa wa kijinsia, mshikamano wa kitaifa na maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.


“Dira hii ni ya  matumaini,imelenga kutoa mwongozo wa namna bora ya kutumia rasilimali zetu kwa maendeleo ya watu lakini hatutaki ibaki kuwa nyaraka ya makabatini, bali chombo hai cha mabadiliko chanya,” amesema Rais Dkt.Samia.

Hivyo ‎ameiagiza Tume ya Taifa ya Mipango kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wanatengeneza nyezo za kupima matokeo (performance measurement tools) zitakazosaidia kufuatilia utekelezaji wa dira hiyo kwa kila ngazi ya Serikali na jamii.

‎Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepongeza uandaaji wa dira hiyo akisema inajikita kwenye mahitaji ya watu, hasa kupitia uwekezaji katika rasilimali watu, usimamizi wa mazingira na usawa wa kijinsia.

‎Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo   amesema kuwa dira hiyo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, na iliridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Juni mwaka huu.

‎“Hii ni dira shirikishi, inayolenga kuweka misingi ya maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho. Imelenga pia kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa ushindani na viwanda una





🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post