MAVUNDE ATOA ANGALIZO KWA WENYEVITI WA MITAA JIMBO LA DOOMA MJINI



Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

 Waziri wa madini na mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini  Anthony Mavunde amewatahadharisha  wenyeviti  wa mitaa yote 222 Ya Jimbo la Dodoma mjini  kuwa waangalifu  wa vifaa alivyowakabidhi  vishikwambi (SMARTPHONE)   ili viweze  kudumu na kufanya kazi iliyokusudiwa ya kurahisisha mawasiliano baina yake na wenyeviti hao wakati ambao kutakuwa na changamoto za kijamii na zakiutendaji kazi .

 

Mhe.mavunde ameyasema hayo katika ofisi ya zamani ya halmashauli ya Jiji la Dodoma, ikiwa  ni hafla ya kukabidhi vishikwambi Kwa wenyeviti wa mitaa  .


"simu hizi zimeunganishwa na mfumo wa kidijitali ambapo zitatusaidia  tuwasiliane Kwa uharaka  zaidi , wewe mwenyekiti wa mtaa kukiwa namatatiza mtaani kwako utakacho kifanya utachukuwa simu yako  utaandika hiyo  changamoto  iliopo mtaani kwako  mfano Kuna mafuliko ya mvua ukiandika tuu kunamafuliko Mimi Moja Kwa Moja ofisini kwangu nitaona hata mkuu wa Wilaya ataona na kuanza kuchukuwa hatuwa haraka za kulitatua hilo janga  ,"amesema.


"nduguzanguni niwaombe kila mmoja akatunze kifaa hiki ninacho mkabidhi ,msifanyie hanasa, tutawasiliana kwa haraka mno inawezekana ukanipigia kwenye simu yangu binafsi nikawa sipatikani wakati huo unatatizo  ukashindwa kunipata   lakini ukitumia simu hii Moja Kwa Moja nitaona ,tuna wachimbaji wa madini milioni tatu ote wakinipigia simu itakuwa siyo rahisi  kuwasiliana Kwahiyo simu hizi mkazitumie vizuri hii ndiyo dunia ya Sasa,".amesema.


kupitia hafra hiyo mavunde amewashukuru  wenyeviti hao na wananchi kiujumla Kwa kushirikiana kikamilifu katika utendaji kazi wake wa uongozi ambapo amehudumu kwa miaka 10 akiwa mbunge   wa Jimbo la Dodoma Mjini.


  "nawashukuru sana sana sina chakuwalipa mwenyezi Mungu atawalipa nduguzanguni kwanzia kesho tarehe 27,2025 sita kuwa kiongozi tena nitakuwa raia wakawaida  namuomba mungu  anirudishe tena  kuendelea kuwatumikia wananchi ,"amesema.


"Kuna watu hapa wanajiuliza  nakabidhi vishikwambi hivi Leo , na leo hii muda wangu wa kuwa mbunge wenu wa Jimbo la Dodoma mjini umeisha wakati huo huo nilisha sema nawania Jimbo la mtumba  wanajiuliza Sasa itakuwaje,niwaambie mfumo huu utaendelea kutumika hata mbunge mwingine atakae kuja kuchukuwa nafasi yangu nitafanyanae mazungumzo ataundeleza mfumo huu wa kidijitali ,"amesema.

 

"Miradi Niliyo iachilia mojawapo ukarabati wa uwanja wa mpira wa miguu wa mtekelezo ,ujenzi wauzio wa hosipitali ya rufaa yamkoa wa Dodoma nitaendelea nayo kamakawaida nikiwa raia wakawaida ", amesema.


kutokana na sheria na taratibu za Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kwa Mujibu wa katiba  , Bunge la Tanzania  linavunjwa Juni 27,2025 hivyo viongozi waliokuwepo madarakani  kuvuliwa  uongozi huo na kuruhusu kufanyika kwa Kampeni kwaajili ya kuwania uongozi mbalimbali Uraisi,Ubunge na Udiwani utakao fanyika Oktoba 2025.









🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post