KATIBU WA UWT ZUZU AJITOSA KUWANIA UDIWANI KATA YA ZUZU


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kata ya Zuzu, Mkoa wa Dodoma, Jenesta Project Malingo, amejiunga rasmi na mchakato wa kisiasa kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya Udiwani wa Kata ya Zuzu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.


Jenesta amekuwa mstari wa mbele katika harakati za kijamii na kiuchumi kwa wanawake wa Zuzu, huku akiongoza miradi kadhaa ya ujasiriamali na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika siasa na maendeleo ya kijamii.


Mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM unaendelea nchi nzima, kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.








🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post