Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT *Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* pamoja na Makamu Mwenyekiti *Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC)* wataanza ziara ya kikazi Mkoani Pwani kuanzia Tarehe 6 Mei 2025 Hadi 15, Mei, 2025, katika kuhamasisha Wananchi Kuboresha Taarifa zao kwenye daftari la wapiga Kura.
Katika Ziara hiyo itakayojumuisha pia Wajumbe wa NEC, Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT, Wananchi watapa Elimu na faida ya kuboresha Taarifa zao ambazo ndizo zitakazotumika katika zoezi la upigaji kura Katika Uchaguzi Mkuu Utakaofanyika baadae Oktoba 2025 kwa kuchagua kiongozi kwenye nafasi ya Urais, Ubunge, na Udiwani atakaewasemea na kutatua kero Mbalimbali zilizopo katika maeneo yao.
Hivyo Wananchi Mkoani Pwani kaeni tayari kuwapokea viongozi wa UWT Katika Maeneo yenu.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.