WAKULIMA WANAENDA KULIMA KILIMO CHA TIJA


Na. Wellu Mtaki, Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Ushirika  Ndug.Godfrey Ng'urah ameipongeza Serikali kupitia  Wizara ya kilimo kwa kuweka mazingira Bora Kwa wakulima ili waweze kulima kwa tija huku akisema  Bajeti ya Wizara ya kilimo imejikita katika sekta ya Miundombinu ya Uzalishaji ikiwemo mbegu,mbolea na pembejeo pamoja na masoko kwa wakulima.


Hayo yamebinishwa jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge mara baada ya bajeti ya wizara ya kilimo kuwasilishwa kwa mwaka wa Fedha 2025/26.


"Bajeti hii imejikita katika kuhakikisha wakulima wengi wanapata mgawanyo uliosahihi wa rasiliamali kupitia bajeti ya wizara ili kuongeza uzalishaji kwa asilimia kubwa kwa watanzania walio wengi na inakwenda kuwasaidia wakulima kulima kilimo Cha tija na kupata mafanikio ".Amesema 


Aidha amesema kuwa uwepo Benki ya Ushirika utasaidia kuchochea uzalishaji kwani wakulima watapata rasimali fedha zitakazowasaidia kufanya shughuli zao kwa kiwango Cha tija na kupata mafanikio Makubwa .


Sambamba na Hayo ameelaza kuwa benki hiyo imejipanga kumuwezesha mkulima pamoja na mfanyabiashara wa mazao kupata huduma Bora na wezeshi Katika bank hiyo.


Ikumbukwe kuwa jengo la  benki ya ushirikiano ilizinduliwa hivi kalibuni na Rais  wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na jijini Dodoma na lipo Square mkabala na jengo la Makao makuu ya chama Cha mapinduzi.

🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post