Na Wellu Mtaki, Dodoma.
Maandalizi ya Mkutano Maalum wa Taifa wa chama Cha mapinduzi (CCM ) umekamilika kwa asilimia 100 na unatarajia kupokea taarifa ya ilani ya uchaguzi na utekelezaji wake,sambamba na uzinduzi wa Ilani ya uchaguzi ikiwemo marekebisho madogo ya katiba ya chama hicho pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Makao Makuu ya chama pembeni mwa jengo la jakaya kikwete.
Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla,wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convetional Centre,ikiwa ni kuelekea Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika tarehe 29-30 Mei 2025.
Amesema ratiba ya mikutano hiyo inaanza Mei 26 kwa kikao cha Kamati Kuu, kikiendelea Mei 28 kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kabla ya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa unaotarajiwa kufanyika Mei 29 na 30.
"Ajenda kuu za mikutano hiyo ni pamoja na kupokea taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, uzinduzi wa Ilani mpya ya uchaguzi kwa pande zote mbili, marekebisho ya Katiba ya Chama pamoja na tukio la uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya jengo jipya la Makao Makuu ya CCM" amesema
Aidha ameeleza kuwa Jengo hilo jipya linatarajiwa kuwa la kisasa na lenye uwezo mkubwa wa kuhudumia wanachama na shughuli za chama, likiwa na kumbi za mikutano na maegesho ya magari, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya muda mrefu ya CCM katika kujenga miundombinu imara inayoendana na ukuaji wa chama.
"CCM ina wanachama zaidi ya milioni 11 nchini na idadi hiyo inaendelea kuongezeka kila siku, hali inayodai ongezeko la uwezo wa kimfumo na kimuundo katika ngazi zote za chama,"Amesema .
Pia Wajumbe zaidi ya 2,000 wa Mkutano Mkuu wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo kwa mujibu wa Katiba ya chama, huku wanachama na wananchi wakihimizwa kufuatilia.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.