MAKALLA: WAJUMBE 2000 KUHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA CCM



Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.


KUELEKEA Mkutano Muu maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa,unaotarajiwa kufanyika Mei29 na 30 Mwaka huu Jijini Dodoma miongoni mwa ajenda za Mkutano huo ni pamoja na marekebisho madogo ya Katiba ya Chama hicho.


Katibu wa itikadi ,uenezi na Mafunzo wa CCM,CPA,Amos Makalla ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema zaidi ya Wajumbe 2000 watahudhuria Mkutano huo. 


Sanjari na hilo,CPA ,Makalla amebainisha kuwa kutakuwa na tukio la uwekaji jiwe la msingi jengo la Makao makuu ya CCM mnamo Mei 288,Mwaka huu jijini humo.


"Jengo hilo jipya linatarajiwa kuwa la kisasa na lenye uwezo mkubwa wa kuhudumia wanachama na shughuli za chama, likiwa na kumbi za mikutano na maegesho ya magari, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya muda mrefu ya CCM katika kujenga miundombinu imara inayoendana na ukuaji wa chama"amesema CPA Makala


Hata hivyo,Katibu huyo wa Itikadi na uenezi na Mafunzo , amesema maandalizi ya Mkutano huo yamekamilika kwa asilimia kubwa.







🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post