TCRA YAWASILISHA RIPOTI YA SEKTA YA MAWASILIANO KWA ROBO MWAKA KUANZIA JANUARI-MACHI 2025,

 


Na Edward Winchislaus, Dodoma.


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ( TCRA) imesema gharama za upigaji wa simu kutoka mtandao moja kwenda mtandao mwingine hazijaongezeka zaidi ukilinganisha na ripoti ya mwaka jana ya sekta ya mawasiliano  kwa robo mwaka ambapo imebainisha kuwa asilimia 99 za watumiaji wa laini za simu hujiunga vifurushi kwanza kabla ya kupiga simu.


Hayo yameelezwa jijini Dodoma  na Mkurugenzi wa masuala ya kisekta kutoka mamlaka hiyo Mha. Mwesigwa Felician wakati akiwasilisha Taarifa ya ripoti ya sekta ya mawasiliano kwa robo tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 kuanzia kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu, ripoti hiyo imewasilishwa kwa waandishi wa habari na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari


Mha.Felician amesema katika ripoti hiyo mamlaka ya mawasiliano Tanzania ( TCRA) imeangazia idadi ya SMS,Dakika na Data zilizotumika katika kipindi cha miezi mitatu ambapo imebaini kuwa idadi ya SMS imeshuka kutoka SMS. Bilioni 52.9 hadi kufikia SMS Bilioni 50.2.


"Majukumu yetu ni kuhakikisha umma unahabarishwa juu ya mwenendo wa mawasiliano na ndiyo maana ripoti hii inawaangazia wadau watatu ambao ni kwanza,Watumiaji,Pili,watoa huduma na Tatu,Serikali.


"Tunaangalia huduma za mawasiliano katika Gharama za kupiga kupiga kutoka mtandao 'A'kwenda mtandao 'A'au  mtandao 'A' kwenda mtandao 'B' ambapo gharama hizo hazijabadilika sana ukilinganisha na ripoti ya mwaka jana,"amesema.






Aidha amesema idadi ya watumiaji wa simu simu nchini imeongezeka kutoka milioni 86 hadi milioni 90.4 sawa na ongezeko la asilimia 4%.Huku katika suala la Internent watumiaji wameongezeka kutoka milioni 48 hadi milioni 49.3.


🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.


Previous Post Next Post