Na Stella Ngenje,Songea.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Wilayani Songea Mkoani Ruvuma Mhe Dkt. Joseph Kizito Mhagama, amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeshiriki Kukuza Uhuru wa Habari hapa Nchini kwa Kutunga Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229 Pamoja na Marekebisho ya Sheria hiyo ya Mwaka 2023.
Mhe. Mhagama ameyasema hayo Jijini Arusha akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari yanayofanyika Wiki hii katika Jiji hilo la Kaskazini mwa Tanzania.
Mbunge wa Madaba akipigilia Msumari kuhusu Ushiriki wa Bunge, ameeleza kwamba Maboresho ya Sheria hiyo ya Mwaka 2023, yanawataka Waandishi wote wa Habari kuwa na Kiwango Cha Elimu Kinachoanza na Taaluma ya Diploma Kwa Kipindi Cha Miaka 5 tangu Marekebisho hayo Kufanyika Mwaka 2023,hatua hiyo itawezesha kuongeza Hadhi ya Tasnia ya Habari hapa Nchini, nakuondoa Ukanjanja Kwenye Tasnia hii Muhimu.
Ikumbukwe kuwa Mhe. Dkt. Joseph Kizito Mhagama Licha yakuwa ni Mbunge wa Jimbo la Madaba, lakini pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala Katiba na Sheria, ni Miongoni mwa Wabunge Wachache wanaoliwakilisha Bunge la Tanzania Kwenye Bunge la Dunia, linaloongozwa na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.