SERIKALI YATENGA ZAIDI YA MILIONI 300 KWA MABWENI YA WATOTO MAALUM SEGESE

 


Na Saida Issa, Dodoma.


SERIKALI imesema kuwa mwaka 2022/23 hadi 2023/24 shule ya Msingi Segese ilipokea shilingi milioni 308 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya watoto wenye mahitaji maalum.


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa TAMISEMI akishughulikia elimu alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Msalala Iddi Kassim Iddi alipouliza Je, lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni ya Watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Segesa.


Alisema kuwa ujenzi wa bweni la wasichana umekamilika, ujenzi wa bweni la wavulana upo hatua za mwisho za ukamilishaji.


"Aidha, kibali cha matumizi ya bweni la wasichana 80 chenye barua ya Kumb. Na. EA.295/315/22/139 kilitolewa tarehe 04/03/2025,


katika mwaka 2025/26 shilingi milioni 323.7 zimetengwa kupitia CSR kwa ajili ya ujenzi wa uzio na nyumba ya mlezi, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji kwa watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo watoto wa Shule ya Msingi Segese kadiri ya upatikanaji wa fedha,"alisema.


🚨Soma HABARI Zaidi katika BlogSpot yetu ya WASHINDI MEDIA.


🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post