RPC KATABAZI AWAFUNDA WANAFUNZI WA VYUO DODOMA KUKABILIANA NA UHALIFU KWA USHIRIKIANO NA POLISI


Na Carlos Claudio, Dodoma.

Wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati mkoani Dodoma wametakiwa kutojihusisha na aina yeyote ya  vitendo  vya uhalifu na badala yake kuwa chanzo cha kutunza amani katika maeneo yao na mkoa wa Dodoma kiujumla kwa kukemea vitendo vyote vya uvunjifu wa amani .


Wito huo umetolewa leo Mei 14,2025 jijini hapa Dodoma  na Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma ( SACP) George Katabazi wakati wa kikao chake  na serikali ya wanafunzi vyuo vikuu na vyakati mkoa wa Dodoma.


Kamanda Katabazi amesema kikao hicho kimelenga kuleta ushirikiano wa karibu kati ya jeshi la polisi mkoa wa Dodoma na wanafunzi wa vyuo vya Dodoma ili kuweza kupambana na vitendo vya uhalifu vinavyo tokea vyuoni na kuwakumba wanafunzi wa vyuo katika mkoa wa Dodoma.


"Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma tunahitaji kuendeleza mapambano dhidi ya uhalifu katika mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na nyie wanafunzi wa vyuo na niwatake tusijihusishe na uhalifu wa aina yeyote kama wizi na utumiaji wa dawa za kulevya bali tukawe chanzo cha kudumisha amani katika vyuo vyetu na maeneo yote ya mkoa wa Dodoma.


"Tunajua kuwa yapo madhara mengi ya kujihusisha na uhalifu au kuwa mharifu utakamatwa na Askari wetu na kuwekwa kifungoni tayari utakuwa ushaanza yataharisha maisha yako,"amesema Kamanda Katabazi.

Pia Kamanda Katabazi amewahimiza wanafunzi hao kudumisha amani,utulivu na usalama katika vyuo vyao na nje ya vyuo kipindi chote cha  zoezi la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi  Oktoba mwaka huu .


Awali akiwasilisha taarifa ya utafiti wa hali ya usalama maeneo ya vyuo Dodoma,ASP Komeya Stephen amesema hali ya uhalifu katika chuo kikuu cha Dodoma ( UDOM) siyo ya kutisha ambapo kuanzia mwezi Juni 2024 hadi Aprili 2025 yameripotiwa matukio kadhaa ya  wizi wa simu, kompyuta, pesa katika ATM za benki , wizi kupitia njia ya mtandao ( tuma kwa Namba hii) na wizi wa vyeti vya shule ya sekondari ambavyo mara nyingi hutumika kuombea mikopo ya wanafunzi.



ASP Komeya Stephen amesema kwa mjibu wa utafiti uliyofanyika katika chuo hicho umebaini kuwa wahusika wakuu wa wizi wa vitu hivyo ni wanafunzi wenyewe,wanafunzi waliyohitimu chuoni hapo na watu kutoka nje ya chuo.


"Hali ya uhalifu siyo ya kutisha sana hususani katika chuo kikuu cha Dodoma ( UDOM) kuanzia Juni 2024 hadi Aprili 2025 yameripotiwa matukio kadhaa ya wizi na wastani wa simu zinazoibiwa kwa mwezi chuoni happ ni 20,Kompyuta 5,na pesa za wanafunzi katika ATM za mabenki pia ule wizi wa mtandao wa tuma kwa namba hii umekuwepo.


"Sababu zinazopelekea wizi huo ni pamoja na tamaa,kukaribusha marafiki kutoka chumba kimoja chi  bweni kwendakuishu chumba kingine na tumebaini kuna udhaifu katika usimamizi wa sheria ndogondogo,"amesema.


Mbali na hayo, Mchungaji Rev. Ivo Livingstone Augustino kutoka St. John’s University aliwahimiza wanafunzi kuendeleza utamaduni wa kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale panapojitokeza viashiria vya uhalifu au migogoro.


Hatua hii mpya inawafanya wanafunzi wa vyuo mkoani Dodoma kuonekana si wahanga tu wa uhalifu, bali pia washirika muhimu katika kulinda amani na usalama ndani ya jamii ya elimu ya juu. 










🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post