NIC YAIMARISHA UELEWA WA BIMA SEKTA YA ANGA KWA MAFUNZO YA KITAIFA JIJINI ARUSHA




NIC imedhamiria kuendelea kutoa huduma bora za bima, sambamba na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kwa lengo la kuongeza wigo wa uelewa wa bima kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.


Ukuaji wa Sekta ya Anga nchini umeendelea kuimarika na kuchochea ukuaji wa uchumi. Kwa kutambua umuhimu wa sekta hii, NIC kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Anga imefanya mafunzo maalum yenye lengo la kubadilishana uzoefu wa namna ya kutazama viashiria vya majanga na kuweza kuzuia, na endapo kutatokea majanga wafahamu namna ya kushughulikia madai.


Mkurungenzi Mtendaji wa NIC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amefungua rasmi mafunzo ya siku tano kwa wadau wa Sekta ya Anga, jijini Arusha.


"Ninawahakikishia huduma bora za bima kwa kuhakikisha madai yote yanalipwa kwa wakati, watendaji wangu wataendelea kushirikiana nanyi na kukiwa na changamoto, tafadhali msisite kuniambia." Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, Mkurungenzi Mtendaji NIC






🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post