MBUNGE MAHUNDI AZITAKA KAMWE MITANDAO ISITUMIKE VIBAYA, AHIMIZA NIDHAMU KWA VIJANA.

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Mbeya, Mhe. Mary Prisca Wilfred Mahundi, ametoa wito kwa vijana kote nchini kutumia vyema fursa zinazopatikana kupitia mitandao ya kijamii, kwa kujifunza, kuburudika na kushiriki katika mijadala ya kujenga taifa, badala ya kutumiwa vibaya au kushiriki katika matumizi mabaya ya teknolojia hiyo.


Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kufungwa kwa Mkutano Mkuu wa siku mbili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Mahundi amewahimiza vijana kuwa na nidhamu ya matumizi ya mitandao, huku akisisitiza kuwa elimu, maarifa na maadili vinaweza kujengwa kupitia majukwaa ya kidijitali.


Aidha, Mhe. Mahundi ametangaza nia ya kurejea kuwania nafasi ya ubunge wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Mbeya, akisema ana imani na uwezo wake wa kuwatumikia wananchi kwa bidii, huku akiwahamasisha wananchi wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.





Katika mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizielekeza Kamati za Siasa za Chama hicho kuhakikisha kuwa zinachuja kwa makini wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani. 


Rais Samia amesisitiza kuwa wagombea wote wanaodai kuwa wametumwa na viongozi wa juu wa chama lazima waondolewe kwenye mchakato wa uchaguzi, ili kudumisha haki, uwazo na heshima ndani ya chama.


Mkutano huo umehitimishwa kwa mafanikio makubwa huku viongozi wakihimizwa kushikamana katika kuandaa chama kuelekea uchaguzi mkuu ujao.



🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post