CHATANDA AKAGUA UJENZI WA KIWANDA CHA KOROSHO - KISARAWE PWANI

 


Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameendelea na ziara yeke ya siku kumi Mkoani Pwani na kukagua Mradi wa Ujenzi wa kiwanda Cha Kubangua na kuuza Korosho katika Kijiji Cha Vilabwa Kata ya Mzenga Wilaya ya Kisarawe ambacho Ujenzi wake unaghalimu Zaidi ya Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia Tisa, (Bil. 2.9) Ujenzi ulioanza Novemba 2024 na kukamilika Novemba 2025 lakini hadi Sasa bado Maendeleo yake hayaridhishi na Kumfanya Mwenyekiti Mary Chatanda kutoa maelekezo kwa wasimamizi wa Mradi huo ukamilike kwa wakati na kuwasihi watendaji wa Mradi huo kuwalipa Vibarua Fedha zao bila kuchelewesha ili kuepusha usumbufu usiokuwa wa lazima.


Aidha Chatanda amewataka viongozi wa Vijiji kuwahamasisha wakulima kupanda miche ya Korosho ya kisasa iliyotolewa na Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Bure na kutumia mbolea za ruzuku kwa kufuata kilimo Cha kisasa ambacho kitawainua wakulima kwa kupata kipato kikubwa na kuinua Uchumi wa Kata ya Mzenga Wilayani Kisarawe.







#UWTImara

#KaziNaUtuTunasongaMbele

#UWTZiaraPwani

🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post