Ibada ya mazishi ya Papa Francis ilifanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, huku Vatican ikitangaza kuwa zaidi ya watu 400,000 wamekusanyika kuhudhuria ibada hiyo ndani ya uwanja na maeneo yanayozunguka.
Kiongozi wa ibada ya mazishi ni Dekano wa Chuo cha Makadinali, Kardinali Giovanni Battista Re. Kardinali huyo Muitalia mwenye umri wa miaka 91 alipata upadrisho katika Jimbo la Brescia mwaka 1957 na Mwaka 2001, Papa John Paul I| alimteua kuwa kardinali.
Kardinali Re alichaguliwa kuwa dekano wa Chuo cha Makadinali mwaka 2020, na Papa Francis aliongeza muda wake katika wadhifa huo mwezi Februari mwaka huu.
Alishiriki katika mkutano mkuu wa makadinali wa Aprili 2005, ambao ulimchagua Papa Benedict XVI, na pia katika mutano muu wa Machi 2013, ambao ulimchagua Papa Francis.
Hivi sasa, Kardinali Giovanni Battista Re anatoa homilia, ambayo inakumbuka maisha na urithi wa Papa Francis.
Akianza hotuba yake, kardinali alisema: "Upendo mwingi ambao tumeushuhudia katika siku za hivi karibuni kufuatia kifo chake kwenda katika maisha ya milele inatuambia ni kwa kiasi gani tumishi mkuu wa Papa Francis uligusa akili na mioyo."
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.