TUTAREJESHA HESHIMA ILIYOPOTEA TUNDURU-ADO

 


Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu, ametoa wito kwa wananchi wa Tunduru kuwa na umoja na kuachana na tofauti zao za kisiasa ili kurejesha heshima ya kihistoria ya wilaya hiyo.


"Hili ninalolisema, Wanatunduru, mnisikilize na tuweke tofauti zetu za kisiasa pembeni. Kabla ya kuja kwa wakoloni, wakazi wa Tunduru, hasa katika himaya ya Wayao, walikuwa kinara wa biashara katika Afrika Mashariki na Kati. Lakini leo, tujiulize, ile heshima ya kihistoria ya Tunduru ipo wapi?" amesema Ado.


Ado ameongeza kuwa leo Tunduru imekuwa wilaya inayonufaisha wachache huku wananchi wake wakipuuziliwa mbali na kunyonywa.


"Mano muri ni hivi karibuni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitisha maoni ya kuongeza majimbo. Halmashauri ya Tunduru, kwa kutojali maslahi ya wananchi, haijapeleka maoni yake. Kwa kufanya hivyo, wameikosesha Tunduru fursa ya kupata jimbo jingine. Kwa maneno mengine, Halmashauri imepuuzilia mbali faida zitakazopatikana na

ongezeko la wabunge, ikiwa ni pamoja na kutanua wigo wa uwakilishi na rasilimali mbalimbali, ikiwemo mfuko wa jimbo," amesisitiza Ado.



"Hili ninalolisema Wanatunduru mnisikilize na tuweke tofauti zetu za kisiasa pembeni. Kabla ya kuja kwa wakoloni, wakazi wa Tunduru kwa maana ya himaya ya Wayao ilikuwa kinara wa biashara katika Afrika Mashariki na Kati, lakini leo tujiulize, ile heshima ya kihistoria ya Tunduru ipo wapi?"


🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post