Nyota wa Ureno na Klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo anaendelea kuitafuta rekodi ya kufunga magoli 1000 baada ya siku ya leo kufunga magoli mawili na kufikisha idadi ya magoli 931 akibakiza magoli 69 pekee kufikia rekodi hiyo.
Ronaldo amefunga katika dakika ya 47 na dakika ya 88 kwa mkwaju wa penati wakati Klabu yake ya Al Nassr ikichuana vikali na wapinzani wao wakubwa Al Hilal katika mchezo wa ligi kuu ya nchini Saudia.
FT: Al Hilal 1-3 Al Nassr
45+4' Al Hasaan
47' 88 Cristiano R.
63' Al Bulayhi A.
Tags
MICHEZO