Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Raia mmoja wa kigeni mke wa mwekezaji mwenza wa Kampuni ya VASO Agreventures ya mkoani Kilimanjaro amemuomba Rais Dr Samia Suluhu Hassan kusaidia kupatikana kwa Haki yake baada ya kunyanyaswa kijinsia na kutolewa kwa nguvu kwenye shamba walilokuwa wanaendesha kilimo cha Maua na Mboga Mboga katika eneo la Kibosho.
Silvia Vlaskamp raia wa Uholanzi na mumewe Alphonsus Nijenhuis wamekuwa wakiishi Kibosho tangu mwaka 2003 ndani ya shamba Hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 170 Mali ya chama cha ushirika Kibosho Kati.
Akizungumza jijini Dodoma na Wandishi wa habari, Silvia alieleza maskitiko yake kunyanyaswa kwa kushikwa sehemu za kifuani na wanaume waliokuja kumtoa shambani bila kuwa na amri yeyote ya mahakama.
Kulingana na Silvia tulip hilo lilitokea 24 Oktoba 2024 nyumbani kwao Kibosho ambapo wanaume hao wakivamia nyumba Yao na kuingia kwa nguvu kisha kupora vitu na kuwatupa nje ya nyumba kama Takataka na kuwaamuru kutoingia tena shambani.
"Siku hiyo nilitaka kuingia kwenye makazi yangu kama kawaida, lakini nilizuiwa na askari ambao hawakuwa sehemu ya Vasso Agroventures. Walinzi hao walinilazimisha kutoka ndani ya gari, wakachukua gari hilo kwa nguvu. Mmoja wa walinzi hao alininyanyasa na kunigusa kimwili licha ya kumwambia mara nne aache kunigusa. Alitaka kuninyang’anya simu yangu wakati nilikuwa nikirekodi tukio hilo. Nilishambuliwa bila sababu yoyote — na ushahidi upo kwenye video."alisema Silvia
Mume wangu alijaribu kwenda kutoa taarifa Polisi Moshi kwa kutumia pikipiki, lakini Polisi hawakujibu simu zozote tulizopiga kuomba msaada. Alipokuwa akiondoka, alishambuliwa na askari watatu wasiojulikana na walimnyang’anya pikipiki yake. Alilazimika kurudi nyumbani kwa usalama wake.
Siku hiyo hiyo, uvamizi haramu na usio halali wa nyumba yetu ulifanyika bila taarifa yoyote, bila notisi, wala amri ya mahakama. Tulifukuzwa kwa nguvu kutoka kwenye nyumba yetu ya kuishi pamoja na shamba letu.
Milango yote ilifungwa. Takriban watu 20 waliovalia kiraia na askari wachache (ambao hawakuwahi kuajiriwa na Vasso Agroventures) walivunja geti na kuvamia kwa nguvu. Mume wangu alipigwa na kutupwa chini. Alielekezwa kutorudi tena kwenye nyumba hiyo. Nilibaki peke yangu ndani ya nyumba.
Walivunja mlango na kuingia kwa nguvu. Askari mmoja aliniambia, naamnukuu: “Ukionekana tena na kamera, kitu kibaya sana kitakupata kwa sababu hufuati sheria zangu.” Nilijawa na hofu kubwa, nikaamua kuweka simu yangu mbali.
Nilikimbilia chumbani kuchukua hati za kusafiria na nyaraka muhimu. Niliweka kwenye mikoba miwili mizito nikaivaa begani. Wakati huo, raia waliovamia walikuwa wanapora mali zangu za binafsi mbele ya macho yangu: pesa taslimu, vito vya thamani, urithi, vifaa vya kielektroniki n.k. Nguo zangu zote zilidhalilishwa na kutupwa barabarani.
Nilipopinga uporaji huo, mwanaume mmoja alinisukuma hadi nyuma ya kabati na kuanza kunigusa sehemu za juu za mwili wangu. Mikoba niliyokuwa nimebeba ilikuwa mizito, sikuweza kujitetea. Nililazimika kupiga kelele kwa nguvu sana nikiomba msaada — lakini hakuna aliyekuja kunisaidia.
Baadaye mwanaume mmoja aliingilia na kumwambia yule mwanamume aache kunigusa — lakini tayari nilikuwa nimeumizwa na kudhalilishwa.
Mali ziliharibiwa mbele yangu:
Vitu vya binafsi vilivunjwa na kuibwa.
Nyumba yangu iliharibiwa kwa makusudi.
Mume wangu alipigwa na kujeruhiwa.
Nikitoka nje, niliona fanicha zetu zikiwa zimevunjwa na kutupwa barabarani kama taka.
Silvia anadai alilikwenda Polisi Moshi kutoa taarifa na maelezo maelezo na kupewa kumbukumbu ya taarifa ya kesi namba MOS/RB/8476/024. .
Hata Hivyo Silvia anadai hadi leo, miezi sita baadaye, hakuna msaada wowote kutoka kwa polisi. Kabla, wakati wa tukio, na baada ya tukio.
Aidha anadai hakuna msaada wowote tuliopata kutoka kwa Polisi wa Moshi. Na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla Hakuna chochote kilichofanyika
Tuliporudi kwenye shamba, askari walituambia tuchukue mbwa wetu 2 na farasi 2 mara moja, la sivyo watawatupa nje kwa nguvu. Ilikuwa hatari sana kwangu kuingia ndani ya nyumba kwa sababu wakati huo walikuwa wameanza kunywa pombe zote zilizokuwa ndani ya nyumba. Walizidi kuwa wakatili na wakorofi.
Tulilazimika kuwatoa farasi kupitia lango la shamba, ambalo liko mbali. Farasi hao walikuwa katika maumivu makali. Ili kuwaokoa, tuliwalazimika kuwapa dawa ya kuwatuliza kabla ya kuwapakia.
Pony 1 alikufa mara tu baada ya kuokolewa. Uchunguzi wa madaktari watatu wa mifugo waliothibitishwa ulionyesha kwamba pony huyo alikuwa na kupasuka kwa viungo vya ndani, uti wa mgongo ulikuwa umevunjwa (C3), na tumbo lilikuwa limejaa damu mpya — dalili zote za kupigwa hadi kufa kwa kifaa kizito butu.
Pony 2 naye alikufa akiwa na majeraha makubwa yaliyoenea mwilini — yaliyokuwa makubwa na ya kina.
Mbwa wawili walilazimika kulazwa kwa dawa baada ya kuonesha dalili za mshtuko na kutetemeka kwa nguvu.
Yote haya yamefanyika kinyume cha sheria, bila hati ya mahakama, kwa nguvu na mateso makubwa dhidi yetu, binafsi na wanyama wetu.
alipoulizwa msingi wa tukio hilo kutokea alidai hisia zake zilijielekeza kuwa wabia wenza kwenye Kampuni ya VASSO ndio huenda wakawa nyuma ya hujuma hizo.
Mapema mwaka Jana baadhi ya vyombo vya habari mkoani kilimanjaro viliripoti kuwepo kwa mgogoro baina ya wawekezaji kwenye shamba hilo ambao walifikishana mahakamani Kuu na kuamuru kampuni hiyo kufungwa.
Hata Hivyo moja wa wakezaji Alphonsus Nijenhuis alikara rural kwenye mahakama ya rufaa na kumpa haki ya kisheria kuendelea kufanya shughuli zake shambani humo.
Wakati kukiwa tayari kuna amri hiyo ya Mahakama kundi la walinzi ndio walivamia shambani na kuwatoa kwa nguvu huku ikisadikika kuwa waliofanya kitendo hicho walikuwa wakitekeleza amri ya mahakama kuu ya awali na ambayo hata hivyo ilikuwa tayari imeshatolewa maamuzi na mahakama juu yaani mahakama ya Rufaa.
Endapo maamuzi hayo ya kisheria yatazingatiwa mwanamke huyo na mumewe watarejeshewa shambani na kuendeleza mkataba wao na chama cha ushirika cha Kibosho Kati unaotarajiwa kukoma ifikapo mwaka 2028
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.