Na Carlos Claudio, Dodoma.
Katika kutekeleza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji Dodoma wamerudisha fadhila zao katika jamii kwa kuadhimisha miaka 61 ya muungano wa Tanzania na kutembelea shule ya watoto wenye mahitaji maalumu iliyopo Buigiri jijini Dodoma
Jeshi hilo la Zimamoto Na Uokoaji Dodoma wamewafikia watoto hao na kutoa misaada ikiwemo mashuka zaidi ya piece 100, kushiriki usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti katika shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1950 chini ya kanisa la Anglikana Tanzania.
Akizungumza na Washindi Media, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji mkoa wa Dodoma Rehema Menda amesema katika miaka 61 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar , Jeshi hilo linajivunia kuwa na mitambo mipya ikiwemo magari katika mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na kuongezeka kwa vituo vya kutoa huduma.
Aidha Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji Dodoma limetoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua taadhari dhidi ya majanga ya moto na kuweka mifumo ya kung’amua uhashiria wa moto.
“Vifaa hivi ni muhimu , juzi tarehe 22 tumeokoa gari lisilopungua thamani ya silingi milioni 40 kwa kifaa kinachobebeka , tukazima moto” amesema Rehema.
Kwa upande wake Simon Jonathan ambaye ni mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema shule hiyo inatoa elimu ya awali kwa watoto wenye mahitaji maalum katika makundi matatu iliwa mtoto asiyeona kabisa, uoni hafifu ikiwa wenye ualbino pamoja na wachache wanaoona ambao wanasaidia wengine.
Sambamba na hayo Mwalimu Simon ametoa pongezi kwa Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji Dodoma kwa kuichagua shule hiyo na kwenda kutoa misaada pamoja na usafi katika mazingira ya shule.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Dodoma kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya shughuli za kijamii kama njia ya kurudisha fadhila kwa jamii. Hili ni jambo muhimu kwani linaonesha mshikamano kati ya taasisi za serikali na wananchi.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.