ELIMU YAPASWA KUTOLEWA, KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA - DKT. NDUMBARO

 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro amesema ili kuwa na jamii yenye uelewa dhidi ya usawa wa kijinsia na kutokomeza Ukatili nchini elimu yapaswa kutolewa kwenye makundi mbalimbali hususani kundi la wanawake ambao hukumbwa na kadhia ya Ukatili kwa kiasi kikubwa.


Akizungumza kwenye Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Mwenyekiti wa UWT Mary Chatanda kwa wajumbe wa Baraza kuu la UWT jijini Dodoma Waziri NDUMBARO akiwa Mgeni mualikwa amesema kupitia mada za  Utawala Bora, Upatikanaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria pamoja na Ukatili wa kijinsia Wajumbe wa Baraza kuu la UWT watapa uelewa mpana juu ya masuala ya Msaada wa Kisheria na watakuwa mabalozi Wazuri wa kutoa elimu kwa kuwafikishia wananchi juu ya elimu hiyo.


Katika hatua nyingine Waziri wa Katiba na Sheria Damas Ndumbaro akawakumbusha wajumbe wa UWT kwenda kutoa elimu kwa wananchi kwenye maeneo yao juu ya kushiriki zoezi la uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwakani kwa kuwa ni takwa la kisheria kwa wananchi kupiga kura kuwachagua viongozi watakaowaletea Maendeleo kupitia chama Cha Mapinduzi, CCM


Kwa upande wa wajumbe wa Baraza kuu waliopata Mafunzo hayo wamesema Elimu hiyo waliyoipata inatoa fursa ya kwao na kwenda kuisambaza Elimu hiyo kwenye maeneo yao ili kupunguza vitendo vya Ukatili wa kijinsia.










🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post