BASHE AZIPIGA MARUFUKU AFRIKA KUSINI, MALAWI KUINGIZA MAZAO NCHINI.

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


 SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, imetoa tamko la kupiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Nchi za Afrika Kusini na Malawi baada ya Nchi hizo mbili kuzuia mazao kutoka Tanzania.


“Wakati mazungumzo yanaendelea sisi hatuwezi kuendelea kuishi kuzuiliwa haki yetu hiyo hivyo natangaza rasmi kuanzia usiku huu mambo yafuatayo kwa Nchi hizi mbili South Africa imekua ikiingiza Tanzania ‘fresh apples’ kwa hivyo kuanzia leo ni marufuku kuingiza fresh apples Tanzania hatutaruhusu zao lolote kutoka South Africa linalohusina na kilimo kuingia Nchini kwetu”


“Kuhusu Nchi ya Malawi mpaka sasa hawajafuta notisi waliyoitoa kwa hivyo ninatangaza rasmi ni marufuku mazao yoyote ya kilimo kutoka Malawi kuingia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo” amesema Bashe.


SERIKALI metoa tamko rasmi la kutoruhusu mazao ya kilimo kutoka nchi za Afrika Kusini na Malawi

kuingia nchini.


Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa tamko hilo rasmi mkoani Dodoma baada ya nchi hizo kutoondoa vizuizi vya mazao ya Tanzania kuuzwa chini humo mpaka jioni ya leo ikiwa ni wiki moja tangu Waziri Bashe kuzitaka nchi hizo kuondoa vikwazo hivyo.


🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post