Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika kuwa Serikali imepokea taarifa rasmi kuwa Serikali ya Malawi imezuia kuingia kwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania, yakiwemo unga, mchele, tangawizi, ndizi, na mahindi.
Hatua ambayo imeathiri moja kwa moja shughuli za
wafanyabiashara wa Kitanzania wanaosafirisha bidhaa hizo kwenda Malawi.
Pia ameongeza licha ya juhudi katika kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kufungua soko la ndizi nchini Afrika Kusini bila mafanikio hali inayofanana na changamoto nchi ilizopigia kwa zaidi ya miaka kumi katika kufungua soko la parachichi, hadi pale Serikali ilipoamua kuchukua hatua za kulinda maslahi ya nchi.
Bashe amesema kutokana na hali hii, na baada ya juhudi zote za kidiplomasia kufanyika bila mafanikio,
- Iwapo Serikali ya Malawi na Afrika Kusini hazitabadilisha msimamo wao kufikia Jumatano ijayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka nchi hizo mbili.
- Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.
3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na watanyabiashara wa Kitanzania.
Hivyo ameshauri wasafirishaji wote wa Kitanzania kuacha kupakia bidhaa za kilimo mpaka hapo Malawi na Afrika Kusini watakapo badilisha msimamo wao.
Pia ameshauri Wafanyabiashara walioweka order za apples, machungwa, na bidhaa zingine ambazo hununuliwa Afrika kusini, kuacha kwa sasa kwani Serikali haitoruhusu kuingia Tanzania mpaka hapo Afrika Kusini itakapofungulia soko la ndizi.
Akisisitiza hatua hizi ni za kulinda heshima ya nchi, uchumi wa wakulima, na usawa katika biashara za kikanda