JENGENI URAFIKI NA WATOTO KUWAJENGEA UWEZO WA KUSEMA CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO


WAZAZI na Walezi wa kata ya Msua mtaa wa Kichangani Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wameshauriwa kujenga urafiki na watoto wao ili kuwajengea uwezo wa kusema changamoto wanazokumbana nazo katika jamii vikiwemo vitendo vya ukatili.

Hayo yalibainishwa May 13,2024 na Asistant Inspecter sponsor Millinga Polisi Kata ya Msua Mkoani humo wakati akizungumza na wananchi hao katika mkutano uliolenga kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi sambamba na maelekezo kutoka ofisi ya halmashauri ya kata ya Msua.

Kamanda Milinga amesema kwa sasa matukio ya ukatili yemekuwa mengi huku akitaja rika la watoto kuwa ndiowanao athirika zaidi.

“Wewe Baba ukiwa mkali unamwadhibu mtoto anapofanyiwa vitendo vya ukatili hawezi kuja kukuambia anakuogopa lakini tukijiweka karibu na watoto wetu,tukiongea na watoto wetu vizuri motto atakuambia kila kitu kibaya alichofanyiwa na mtu yeyote.

“Mtoto ametoka shuleni badala ya kumpa chakula ale wewe tayali unaanza kumfokea unaanza kumpiga kwahiyo motto anapofanyiwa ukatili anashindwa kukuambia lakini kama tutakuwa karibu na watoto kila kitu atakachofanyiwa atasema kwa Baba na Mama tusiwapige sana ,tusiwagombeze sana watoto wetu,”alisema Kamanda Milinga.

Sanjari na hayo amewataka wananchi hao kuacha kuwakaribisha wapiga ramli chonganishi (Lambalamba) na kuwataka kutambua athari zake huku akiainisha baadhi ya athari hizo ikiwa ni pamoja na kuvuruga amani katika familia na jamii kwa ujumla,kuibiwa pesa bila ya wao kujua.

“Hawa lambalamba jamani sio watu wazuri ninaombeni sana katika mtaa huu wa kichangani akitokea mwananchi mmoja akasema jamani hapa hatulali usiku hapa sijuwi kuna waganga,wachawi tuwalete waganga msikubali tena mkamateni mleteni kwangu kwa sababu huyo anataka kuharibu amani ya mtaa wenu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya kilimo na afya ya jamii Tanzania Mkoa wa Rukwa Bw.Leonard Mwanjisi alisema kuna utaratibu wa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na kuanzia ngazi ya mtaa,kijiji,kata,wilaya hadi ngazi ya mkoa huku akiwataka wazizi kuacha kasumba ya kuwafungia watoto majumbani.

Mwanjisi aliwasihi wazazi kuacha kuwa vichocheo vya kuwakatisha tama watoto na hivyo kusababisha utoro mashuleni kukithiri kwa kuwafanyisha shughuri za shambani badala yake kuwahimiza kupambania ndoto zao za badae.

“Kuna familia hapa kazi yao ni kupiga tu watoto hamuelekezi kwamba nakupiga kwa nini,mtoto anaelekezwa na kufundisha unavyompiga mtoto kwamba umemukuta kwenye video mwambie kwanini video ni vibaya,usimpige tu mimi sitaki video wakati anaona watu wanashughurika navyo. 

Kupitia mkutano huo aliwaasa wazazi kuwa na contro ya kufanya baadhi ya vitu mbele ya watoto jambo linalopelekea watoto kufanyiwa ukatili wa kihisia,kisaikolojia na kuwataka akina baba kuacha kuwafanyia ukatili wamama wajawazito.

Mwandishi Fedrick Mbaruku

Muhariri Edward Winchislaus

MWISHO. 

Previous Post Next Post