ACHENI KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA,LINDENI WATOTO DHIDI YA UKATILI-MWANJISI

Katika kuunga juhudi za Serikali za kukabiliana na vitendo vya ukatili nchini Wananchi wa Kata ya Msua Mtaa wa Mkuyuni Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wamepatiwa elimu juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya, unywaji wa pombe kupindukia sambamba na elimu ya utunzanji wa vyanzo vya maji kwa kuacha kufanya shughuri za kilimo kando na vyanzo vya maji.

Akizungumza na wananchi wa mtaa huo May 5,2024 Mkurugenzi washirika la maendeleo ya kilimo na afya ya jamii (ADEACH) Bw.Leonard Mwanjisi alisema elimu imekuwa ikitolewa kwa wakazi wa mkoa huo kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na shirika ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya afya,kupinga matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Mwanjisi aliwataka wananchi hao kuondokana na matumizi ya vilevi na kujua athari zake zinazoweza kupelekea kukithili kwa vitendo vya ukatili.

“Unapokuwa unatumia vilevi,madawa ya kulevya kuna vitu vinaathiri mwili wako kuna muda utaanza kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida kwahiyo unaathirika kisaikolojia.

“Angalia Yule mtu aliye athirika kisaikolojia anamke anawatoto na umri wao umefika kwenda shule lakini hawajaenda shule kwa nini ? Ule upeo wa kufikiri umepungua,mbali na kupata magojwa ya akili akiwa ni muathirika wa dawa za kulevya ni rahisi pia kupata ajari awapo barabarani,”alisema Mwanjisi.

Pia Mwanjisi alizitaja athari hizo ikiwa ni pamoja na kupunguza nguvu kazi ya taifa,ajari zisizotarajia,ongezeko la watoto waishio katika mazingira magumu,ndoa nyingi kuvunjika,watoto kukosa haki yao ya kielimu,ukatili kwa watoto,kupunguza uzalishaji katika familia jambo linalo changia kudidimiza pato la taifa.

Kwa upande wao wananchi wa mtaa huo walihoji kuhusu uelewa wao juu ya vyanzo vya maji na kupatiwa majibu huku wakiiomba serikali kufanyia ukarabati katika maeneo yanayotajwa kusababisha vifo kwa watoto wao.

Hata hivyo wanaojishughurisha na kilimo kandokando ya vyanzo vya maji walishauriwa kuacha hatua kadhaa kutoka katika chanzo cha maji ili kuendelea kulinda vyanzo hivyo.

Akijibu swali la kiongozi wa mtaa huo aliyetaka kujua ni sifa zipi zinazo kitambulisha chanzo cha maji? Mwanjisi alisema zipo sifa zinazoweza kukitambulisha chanzo cha maji “Ili tuite mto lazima luwe na sifa mara nyingi sana kitu kinachoitwa mfereji unaweza ukatumika kupitishia maji yanayotoka sehemu Fulani,tunapo zungumzia chanzo ni pale kitu kinapotokea inaweza ikawa ni chemchemi baadae nyie mnaoishi eneo lile mnavyofanyia shughuri zenu pale mkapafanya mkakuta pamebadilika na kuwa kitu kingine.

Previous Post Next Post