Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuimalisha miundombinu ili kuendeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Dk.Samia ameyasema hayo leo Mei 13 mwaka huu katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo Dk.Samia amesema ahadi ya serikali katika kukuza na kuimalisha sekta ya mawasiliano itsaidia kutoa frusa za ajira kwa vijana na kuchoche maendeleo nchini.
Amesema kuwepo kwa huduma bora za mawasiliano hususani vijijini ni muhimu katika sekta za kiuchumi,kisiasa,kijamii,kiutamaduni na kiulinzi.pamoja na usalama wa nchi.
Dk. Samia amesema kutokana na kuongezeka na kuboresha huduma ya mawasiliano hali hiyo itachochea mafanikio katika kukuza sekta hiyo ili kufikia adhima ya serikali.
"Tunaenda kukuza sekta ya mawasiliano kwa sababu huduma zikiwepo changamoto zote za mawasiliano zinaenda kuisha lakini kubwa zaidi tunaenda kubadilisha teknolojia vijijini na tutakapo imalisha upatikanaji wa huduma hii wakulima wanaenda kutoka kwenye tocho wanakwenda tachi kwa sababu hizo tachi ndizo zitzwapa taarifa za nchi na kidunia,"Dk.Samia
Dk.Samia amesema mbali na hayo huduma za kimtandao zitaenda kuisaidia serikali kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Amesema mradi wa Mmama ambao ulianziashwa nchini na sasa unatumiwa na nchi nyingine za Afrika unaotua mtandao katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Hata hivyo Dk.Samia amezipongeza kampuni za mawasiliano ikiwemo Vodacom,TTCL,Halotel,Airtel na Tigo kwa huku akiseama Tanzania inauwanda mpana wa watu wanaotumia mitandao mbalimbali katika kutuma na kufanya miamala ya fedha kupitia simu.
Pia Dk.Samia amesema miradi hiyo ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi inayotoa mshukumo mzuri wa maendeleo na kuziomba sekta nyingine kuendana na mfumo huo.
Amesema utekelezaji wa mradi huo hatua mhimu katika kuuelekea mapinduzi ya nne ya maendeleo ya viwanda ambavyo msingi wake ni kufikia uchumi wa kisasa.
Pamoja na hayo amesema mtandao wa mashirika ya simu umetoa fedha ili kusaidia mradi huo kukamirika kwa haraka katika suala la uwekezaji huku akisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kukuza pato la Taifa kutokan na kuongezeka kwa wigo wa teknoloji ya habari na mawasiliano na tehema pamoja na mawasiliano katika sekta nyingine.
Amesema kuwa kwa mjibu wa sens ya watu na makazi ya mwaka 2022 ripoti zinaeleza kwamba usikivu wa simu katika maeneo ya vijijini hadi sasa umeongezeka na kufikia asilimia 97 ukilinganisha na asilimia 45 za mwaka 2009.
Katika hatua nyingine Rais Samia amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa umeme katika maeneo ya vijijini pamoja na utaratibu wa taasisi mbalimbali katika utoaji wa vibari na kuzitaka mamlaka husika kufanya mapitio ya utoaji wa v ibari ili kuondoa adha kwa wananchi.
"Vibari visizidi mwezi mmoja havija toka,mwezi mmoja viwe vimetolewa si zaidi ya mwezi mmoja kuanzia leo tarehe 13 mwezi huu hadi mwezi june 13 nitakuliza waziri mmekwendaje?mmekwama wapi na nani kakwamisha ?kwa hiyo wale wenye makoti mazito nitawaambia wavue ili mikono iwe miepesi kutoa vibari hivyo,"Dk.Samia