Agosti 15 2026
Kila Ifikapo Angosti 15 kila mwaka ni kumbukizi muhimu sana kwangu kwa siku ya kuzaliwa kwangu Mr Barnabas Kisengi aka Babu
Napenda kumshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kunijalia uhai na Afya njema kwa kuiona tena siku ya Leo ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu
Pia Napenda kuwashukuru sana wazazi wangu kwa kunilea katika Maadili mema na mzuri hadi kufikia hapa nilipo Sasa
Bila kuwasahau Napenda kushukuru sana familia yangu Mke Faustina na wangu Jemsi, Pendo, Sharon, Vanessa na Brian kwakuweza kunipa Utulivu katika maisha yangu yote hadi kufika Siku hii ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu hakika wamenipa ushirikisno mkubwa sana katika maisha
"Hakika Maisha ni safari ndefu yenye mito na mabonde hivyo ukiona umefikia hadi Sasa kufika umri huu napaswa kushukuru sana mwenyezi Mungu na wazazi wangu na familia yangu kwa kuhakikisha nimeziona tena kumbukizi yangu ya kuzaliwa Angosti 15 ni safari ndefu iliyojaa matumaimi makubwa kuiona Siku hii Muhimu sana katika maisha yangu"
"Pia Napenda kumshukuru sana Mke wangu Mpendwa Faustina amekuwa karibu nami muda wote kuhakikisha napata Utulivu wa afya na kuwa I mara katika maisha yangu yote huwa nashindwa hata nimuite jina gani zuri maana huwa ananofanya niwe na amani na baraka tele katika maisha hivyo hunifanya nimpende sana Mke wangu hakika yeye ni nyota yangu,kipenzi changu, kidani cha moyo wangu kwa kuhakikisha ananipa utulivu wa kutosha na kuhakikisha niko salama hadi siku ya leo tena kwa kuwa Maisha Bora yenye furaha,amani na Utulivu tele katika maisha yangu hakika nampenda sana Mke wangu Mpendwa Bi Faustina aka Mrs Kisengi (Babu) hakika wewe ni waridi wa Moyo wangu Mwamba wangu,Mpambanaji wangu wa Maisha Nampenda sana zaidi ya sana Mke wangu Faustina na Familia yangu"
Aidha Napenda kuwashukuru watu wote ndugu zangu, jamaa na marafiki wote hakika mmekuwa nuru na muhimu kwangu hadi kufika siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu
Happy birthday to you Mr Barnabas Kisengi aka Babu.
Mwenyezi Mungu aendelee kunipa Afya njema katika maisha yangu.












